NINI
MAANA NA CHIMBUKO LA TPIF
Tanzania Peace Initiative Foundation ni
asasi ya kiraia iliyo sajiliwa kisheria kwa upande wa Tanzania bara asasi hiyi
ili sajiliwa chini ya kifungu cha 12(2) Act No 24 ya mwaka 2002, na Namba yake
ya usajili ni 00NGO/00006106. Kwa upande wa Zanzibar asasi hii ilisajiliwa kwa
sheria namba 6 ya mwaka 1995.
Asasi hii imeanzishwa kutokana na hali ya
amani ya nchi ya Tanzania kuonekana kuwa ustawi wake unazorota, tathmini hii
ilifanyika kwa kuwashirikisha wadau mbali mbali wenye uelewa katika maswala ya
amani ya nchi hasa wale walio somea maswala ya husuyo utatuzi wa migogoro na
ujengaji wa amani, wanasiasa wakongwe na wazee wanao ijuwa historia ya Tanzania
tangu ipate uhuru wake mwaka 1961.
Ustawi wa amani huendana na maendeleo ya
kisiasa kiuchumi na kijamii; ustawi wa amani hubeba dhana ya kurithishwa; tena
machafuko ni adui wa hayo yote na zaidi sana huwaathiri watoto na wanawake.
Kutokana na uchunguzi huo wa kina
uliowahusisha wataalam wa maswaala ya utatuzi wa migogoro na ujenzi wa amani
wenye ueledi, TPIF ilibidi kuzaliwa na kusajiliwa kisheria ili kuweza kuiarifu
jamii kwa kutoa elimu na kuisemea amani kuhusu ustawi wake nchini.
MALENGO
YA TPIF kwa ufupi
MALENGO/MADHUMUNI
1.
Kuelimisha
na kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa amani na maendeleo kwa jamii
2.
Kurahisisha ujenzi wa amani kwa kushajihisha
haki za binaadamu na demokrasiya.
3.
Kurahisisha utatuzi wa migogoro na kuidhibiti katika
jamii, taifa na kimataifa.
DHANA
YA VIKUNDI VYA AMANI
Moja kati ya mbinu ama njia iliyo ridhiwa
kuwekwa kwenye kutimiza azima ya TPIF kuisemea amani ni kufungua vikundi vya
amani ambavyo vitatumika kama vyombo vitakavyo isemea amani ya Tanzania kwa
kuigusa jamii kwa ukaribu zaidi ili kukuza ustawi wa amani yetu kwa ujumla.
Vikundi hivi vya amani vitafunguliwa
kwenye mikoa ya nchi nzima ya Tanzania ambapo mpango huu utatekelezwa kwa awamu
ukianza na Zanzibar, Dar-Es-Salaam,
Mwanza, Tabora, Morogoro, Pwani, Arusha, na Mtwara
Masharti
ya pamoja ya kujiunga na vikundi vya amani
Mtu
yeyote alie ni mtanzania, mzalendo tena mpenda amani anaweza kujiunga na
VIKUNDI VYA AMANI kama mtu wa kujitolea bila ya pingamizi bali tu awe amekidhi
vigezo vilivyo ainishwa kwenye kipengele hiki. Na niutaratibu kuwa ili mtu awe
mwanachama au mtu wa kujitolea (Volunteer) halisi basi mtu huyo imempasa ajaze
fomu nakupitiwa na uongozi wa TPIF ili kuungwa kuwa kama alivyo kusudia
mwenyewe. Taasisi hii haita athiri muda wa kujitafutia maendeleo kwa mtu yeyote
atakae jitolea bali kwa ridhaa yake, utashi, na uzalendo wake mwenyewe.
FAIDA
ZA KUJIUNGA NA vikundi vya amani
1.
Mwanachama yeyote atakae jiunga na vikundi
vya amani atapata fursa ya kuhudhuria makongamano, seminars na workshorp mbali
mbali zitakazo endeshwa na TPIF ama asasi yeyote ya kiraia yenye uhusiano na
TPIF.
2.
Mwanachama atapata kuunganishwa na
vikundi vya wajasiriamali wazoefu; mabenki yenye mikopo ya riba nafuu; na
wizara zenye mipango na Vijana kwa kundi la Vijana. Ijapokua lika la mtu
halitoathiri fursa ya mtu yeyote katika kutimiza azma ya amani na maendeleo.
3.
Mwanachama atapata haki ya kulipwa katika
kila semina, kongamano, au workshop yeyote itakayo endeshwa kwa malipo.
4.
Mwanachama atatapata fursa ya kutembea ndani
na nje ya nchi ili kuzidi kujifunza.
SERA YA UTEKELEZAJI
MAJUKUMU
Asasi
hii inazingatia kua, kila mtu atatekeleza wajibu wake bila ya kuvunja sheria za
nchi wala taratibu zozote zilizowekwa kisheria. Tena shughuli za vikundi hivyo
havitatakiwa kuharibu shughuli binafsi za mwanachama katika utekelezaji wake wa
majukumu.
Washiriki
1.
Kituo
cha utafiti na utatuzi wa migogoro cha Africa
IMAMU
M. VUAI
TPIF
EXECUTIVE SECRETARY
No comments:
Post a Comment