Wasio na uwezo kusaidiwa kisheria
Wizara ya Katiba na Sheria imesema inaandaa sheria ya msaada wa kisheria bila malipo ili kuwasaidia wananchi wasio na uwezo katika mashauri ya jinai na madai.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa Wizara ya Katiba na Sheria, Farida Khalfan, alisema kutungwa kwa sheria hiyo kunafuatia kilio cha muda mrefu cha wananchi ambao wamekuwa wakipata shida katika kupata haki kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.
"Maandalizi ya muswada kwa ajili ya sheria hiyo yapo katika hatua za mwisho serikalini kabla ya kuwasilishwa katika Bunge. Lengo la serikali ni kuwa ifikapo Januari, 2014 sheria hii iwe imekamilika," alisema.
Alisema pamoja na mambo mengi, sheria itakayotungwa itaunda chombo huru kitakachokuwa na majukumu mbalimbali, ikiwamo kusajili taasisi zinazotoa msaada wa kisheria nchini pamoja na kusajili watoa msaada wa kisheria.
Pia alisema chombo hicho kitaweka viwango vya ubora katika utoaji misaada ya kisheria na kuvisimamia viwango hivyo, kusimamia nidhamu na maadili ya watoa huduma za msaada wa kisheria, kutambua wasaidizi wa kisheria na kutafuta fedha ili kutekeleza majukumu yake.

No comments:
Post a Comment